Luke 18:35-40

35 a bIsa alipokuwa anakaribia Yeriko, kipofu mmoja alikuwa ameketi kando ya njia akiomba msaada. 36Kipofu huyo aliposikia umati wa watu ukipita, akauliza, “Kuna nini?” 37 cWakamwambia, “Isa Al-Nasiri anapita.”

38 dAkapaza sauti, akasema, “Isa, Mwana wa Daudi, nihurumie!”

39 eWale waliokuwa wametangulia mbele wakamkemea, wakamwambia akae kimya. Lakini yeye akapaza sauti zaidi, “Mwana wa Daudi, nihurumie!”

40Isa akasimama, akawaamuru wamlete huyo mtu kwake. Alipokaribia, Isa akamuuliza,
Copyright information for SwhKC